WAWEKEZAJI KUTOA KIPAUMBELEA CHA AJIRA KWA WANANCHI

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania kassim majaliwa amewataka wawekezaji kutoa kipaumbelea cha ajira kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya karibu na maeneo yao ya uwekezaji ikiwemo viwanda.
Akizungumza alipotembelea kiwanda cha saruji cha lake amewasisitiza wawekezaji hao kulipa kodi kwa wakati na kuwapongeza kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kuifanya tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.
waziri mkuu mjaliwa pia ametembelea kiwanda cha nyuzi cha namera na kiwanda cha nguo cha nida jijini dar es salaam na kueleza kuwa watanzania wanaweza kuachana na nguo za mitumba muda si mrefu kutokana na ongezeko la viwanda vya kutengeneza nguo nchini.
Amesema kutokana na mafaniko hayo hakuna haja ya pamba inayozalishwa nchini kuuzwa nje ya nchi kwa sababu lipo soko la uhakika na kuwataka wakulima kulima zao hilo kwa wingi.