WAWEKEZAJI WAZALENDO KUANZISHA VITUO VYA AFYA NA KUTOA HUDUMA NAFUU KWA WANANCHI ZINAPASWA KUUNGWA MKONO.

Waziri wa afya mh. Mahmoud thabit kombo, amesema jitihada za wawekezaji wazalendo za kuanzisha vituo vya afya na kutoa huduma nafuu kwa wananchi zinapaswa kuungwa mkono.

Akizindua kituo cha dr. Amesh mehta hospital katika kijiji cha nungwi, mh. Thabit kombo, amependekeza kuwa utoaji wa huduma uendane na dhamira kuu ya sera ya afya ya kutoa huduma kwanza kwa mgonjwa ili kuokoa maisha yake.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo dr. Amesh mehta, amsema gharama iliyotumika kwa ujenzi na vifaa vya kisasa vya matibabu ni dola laki moja na hamsini za marekani, na amefanya hivyo kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma ya afya kwa wananchi wenzake wa zanzibar.

Baadhi ya watendaji wa hospitali hiyo wamesema kituo kitafanyakazi kwa saa 24 kwa vile kina vifaa vya kisasa na dawa za kutosha kuhudumia wakaazi wa nungwi na wageni wanatembelea kijiji hicho.