Watu wawili wakaazi wa konde wilaya ya Micheweni wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa kaskazini pemba, baada ya kukamatwa na magunia 18 ya karafuu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18, yaliyokuwa katika harakati za kusafirshwa nje ya nchi kinyume na sheria.
Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba kamishna msaidizi mwandamizi , Mohammed Skhekhan Mohammed , amesema tayari jeshi hilo limefungua jalada, na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba Mhe Omar Khamis Othman amesema kwamba kutokana na wingi wa karafuu, zinaonyesha kwamba ni za msimu wa mwaka jana, kwani kwa mwaka huu, bado uchumaji wa karafuu hajafikiwa kiwango hicho.
Naye mdhamini wa shirika la biashara la taifa zanzibar ofisi ya pemba Abdalla Ali Ussi , amesema kwa mujibu wa sheria ya maendeleo ya karafuu, hairuhusu mwananchi kuhifadhi karafuu nyumbani kwake na kuomba sheria zichukue mkondo wake.