WAZALISHAJI WA BIDHAA WATAKIWA KUZITUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI ILI KUJILETEA MAENDELEO

 

Wakala  wa maendeleo  ya viwanda  vidogo   vidogo,   vidogo  na  vya  kati ( smida)   imewataka  wazalishaji wa bidhaa mbali mbali   kuzitumia  fursa  zinazotolewa  na serikali  katika  kujiletea maendeleo ikiwemo kuitumia   maendeleo.

Akiwasilisha kanuni za kuongoza mfuko wa maendeleo ya viwanda vidogo vidogo, vidogo na vya kati, kwa wadau mnali mbali, mkurugenzi  mkuu wa  wakala  wa  maendeleo  ya  viwanda  vidogo  vidogo, vidogo  na  vya  kati, nd.  Haji  Abdul-hamid  amesema   smida  ina lengo  la  kuwaweka  pamoja  wazalishaji  wadogo  wadogo  na wa kati  na kuwajengea  mazingira  ya kuweza kuzalisha  bidhaa  zenye ubora , viwango  na usalama  zitakazoweza  kuuzika  ndani  na  nje  ya  nchi.

Aidha  amesema  smida  imejipanga  kutoa  mikopo  na  huduma  ya  upatikanaji,  ununuzi,  na  usambazaji  wa  vifungashio  kwa  wazalishaji wa  bidhaa,  ili  bidhaa  zao  ziweze  kuwavutia  watumiaji  na  kuuzika  kwa  urahisi.

Mwanasheria  wa  wakala  wa  maendeleo  ya  viwanda  vidogo  vidogo, vidogo  na  vya  kati  nd.  Ali  salum  ali  ametoa  wito  kwa  wananchi  kukitumia   vyema  chombo  hicho  kwa  kutatua  matatizo  yanayowakabili  ikiwemo  upatikanaji  wa vifaa vya  kutendea  kazi    pamoja  na kupata  huduma  za  vipimo  vya  maabara,   ili  kuthibitishwa  kwa  ubora  wa  bidhaa  zao.