WAZAZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU ILI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WANAFANYA VIZURI KATIKA MITIHANI YAO

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh,riziki pembe Juma amewahimiza wazazi kuendelea kushirikiana na Walimu ili kuhakikisha wanafunzi wa zanzibar
Wanafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari afisini kwake mazizini kuhusiana na matokeo ya mtihani wa kidato cha sita ya mwaka 2017, kwa skuli za zanzibar, riziki amesema jumla ya wanafunzi 1,260 sawa na asilimia 88.98 wana uwezo wa kuendelea na masomo katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi, ukilinganisha na asilimia 85.6 ya mwaka 2016.
Aidha amesema wanafunzi 157 sawa na asilimia 11.01 watakuwa na uwezo wa kujiunga na vyuo mbali mbali kwa ngazi ya stashahada.nae naibu waziri wa elimu mmanga mjengo mjawiri amesema wizara inaanda mikakati zaidi ya kuwapa taaluma walimu wake ili kuwajengea uwezo zaidi wa kusomesha wanafunzi maskulini.