WAZAZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU KATIKA KUHAKIKISHA MTOTO ANAANDALIWA VYEMA KATIKA UPOKEAJI WA ELIMU

 

wazazi  na  walezi  wamesisitizwa  kushirikiana  na  walimu  katika  kuhakikisha  mtoto  anaandaliwa  vyema  katika  upokeaji  wa  elimu  ili  kumuwezesha kufanikisha malengo  yake  ya  baadae.

hayo  yamebainishwa  na  uongozi  wa  jumuiya  ya wanawake wanaojishuhulisha na malezi makuzi  na  maendeleo  ya mtoto awopac walipowatembelea  na  kuwapatia vifaa  vya  skuli watoto wanaoishi  katika mazingira  magumu  waliopo  katika  skuli  ya  mkwajuni wamesema  umefika  wakati  wa  kuwaandalia  mazingira mazuri   watoto  hao  ili  waweze  kumudu  vyema harakati  za  maisha yao.

wamesisitizia  suala  la  kuwa  karibu  na  watoto  hao  ili  kuweza  kusema  yanayowakwaza kwa  kuyapatia  ufumbuzi  ili  lengo  la  serikali  juu  ya  upatikanaji  wa  elimu  kwa  watoto  wote  nchini  liweze  kufikiwa.

makamu  mwenyekiti  wa  jumuiya  hiyo   khadija  rajabu  akizungumzia  vitendo vya  udhalilishaji  wa  watoto   vinavyojitokeza  siku  hadi  siku  ni  vyema  jamii  kulipa  kipaumbele  kwa  kuwafichua  wahalifu  ili  kuwawezesha  watoto  kufikia  ndoto  zao.

afisa  elimu  wilaya  kaskazini  a  kheir makame  amewataka  wazazi  kushajihishana kuwapeleka watoto skuli  kuanzia  umri  wa  miaka  minne  ili  waweze  kupata  haki  yao  ya  msingi  na  kuachana  kisingizio  cha  halingumu  ya  maisha  kutokana na elimu  hiyo  hutolewa  bure kuanzia  ngazi  ya  maandalizi