WAZAZI KUTOFANYA MZAHA JUU YA SUALA LA KUWAPATIA ELIMU WATOTO WAO

 

Mwakilishi wa jimbo la chumbuni mhe, miraji kwanza amewataka wazazi kutofanya mzaha juu ya suala la kuwapatia elimu watoto wao ili kuwajengea maisha bora hapo baadae.Mhe, miraji ameeleza hayo katika hafla ya kuwakabidhi zawadi wanafunzi waliofaulu mitihani ya taifa na walimu waliostaafu katika skuli ya mwembemakumbi.

Amesema hakuna jambo zuri zaidi ya mzazi kumuwekezea mtoto wake katika elimu na kuongeza uongozi wa jimbo la chumbuni utaweka kipaumbele suala kuimarisha miundombunu ya skuli ili kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.Mwakilishi wa jimbo la magomeni mhe, rashid makame shamsi ambae alihudhuria hafla hiyo amesifu wanafunzi wa jimbo la mwembemakumbi kwa kufanya vizuri katika mitihani ukilinganisha na wanafunzi wa jimbo lake na ametoa msaada wa vifaa vya kusomea.Mkurugenzi wa baraza la manispaa mjini ndugu aboud mohammed sengenge amewata wazazi kuwa makini na watoto wao wa kiume ambao inaonekana sasa hawapendi kusoma ukiinganisha na watoto wa kike.