WAZAZI KUWA KARIBU NA WATOTO WAO KWA KUWADADISI MASUALI MBALI MBALI

 

Mkuu wa wilaya ya mjini marina joeseph tomas  amewasisitiza  wazazi  kuwa  karibu sana na watoto wao  kwa kuwadadisi  masuali mbali mbali  ili kupata uhakika  wa  kwenendo  wao na tabia.

bibi marina ameyasema hayo wakati wa kuwatunuku zawadi  watoto  na walimu wao huko katika  kanisa latanzania asemble of gold kariakooo kwa niaba ya mkuuu wa mkoa wa mjini magharib mh  ayoub  mohamed mahamod  ikiwa ni kusherehekea kwa  skuuu ya x-mass  kwa kuzaliwa yesu kisto    ambapo madhehebu mbali mbali ya  dini hiyo ya  kikiristo  wamejumuika pamoja.

Amesema ni vizur wazazi na walezi  kuwa wangalifu kwa watoto wao  kutokana na kuwepo  vitendo vya ubakaji vinavyofanywa na badhi ya watu  wasiowatakia mema  jamiii.

nao  wachungaji  wa makanisa  mbali mbali  wameushukuru  uongozi wa serikali  kwa kuendesha ibada zao kwa furaha  na kusherehekea skuuu hiyo   kwa amani na utulivu .