WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO VITUO VYA AFYA KWA AJILI YA KUPATIWA CHANJO

 

 

Daktari dhamana wa  wilaya ya kaskazini “a”  dk Himid Juma  Saidi amewataka wazazi wa wilaya hiyo kuwapeleka watoto  vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa chanjo ili kuwaepusha na maradhi watoto wao.

Akizungumza na wajume wa kamati za afya za shehia za tumbatu kwa wakati  mbalimbali mganga huyo amesema wakaazi wa  wilaya ya kaskazini “a” baadhi yao hawana muwamko wa  kupeleka watoto kupata  chanjo jambo ambalo linashusha kiwango cha watoto wanaopata chanjo wilaya hiyo, amesema vituo vilivyo na ripoti ndogo ya chanjo ni chaani kubwa, tazari, nungwi, tumbatu gomani na tumbatu uvivini.

Dkt himidi  amesema kwa mwaka 2016 walitarajia kuchanja watoto 5039 na badala yake walichanja watoto 3727  hali ambayo  inaweza kusababisha kutokea  kwa marazi ya huharo , pepopunda, porio na surua

Daktari dhamana wa kituo cha tumbatu gomani mcha haji makame amesema  mila za wakaazi wa tumbatu za kutokutolewa nje mtoto mara tu anapozaliwa mpaka atimize siku harobaini nichangamoto kubwa inayosababisha kutofikia lengo la kuwapa chanjo watoto  kwa  wakati katika kituo hicho.

Sheha wa shehia ya tumbatu uvivini hassan  mwadini haji amesema  serikali inafanya juhudi za kuwaelimisha wakaazi hao ili kuondosha tatizo hilo.

Zoezi la chanjo la mtoto wa afrika lita anza tarehe kesho na ujumbe wa mwaka huu ni jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya.