WAZAZI NA WALEZI KUWAKATAZA WATOTO WAO KUJIHUSISHA NA BIASHARA

 

Waziri wa wizara ya kazi Uwezeshaji Wanawake na Watoto mhe, Moudline Castico amewataka wazazi na walezi kuwakataza watoto wao kujihusisha na biashara zisizorafiki nao ili kuwajengea mustakbali mzuri wa maisha yao ya baadaye.

Ametoa wito huo huko bustani ya uwanja wa ndege wa Karume kisiwani Pemba alipofanya ziara fupi ya kuangalia watoto wanaojishughulisha na biashara ikiwemo uuzaji wa mabungo jambo ambalo huwakosesha kuitumia vyema haki yao ya msingi ya kupata elimu

Amesema  wazazi na walezi  lazima washirikiane  katika  kuwakataza watoto  kufanya biashara zisizostaki  na badala yake wawatilie  mkazo  katika masoma ili kutimiza ndoto zao

Wakizungumza watoto hao wamesema wanafanya biashara ya kuuza mabungo na vitu vingine kutokana na halingumu ya kiuchumi katika familia zao au wakati mwingine  kutumwa na walimu wao wa madrasa ambao halipwi mshahara

Z B C ilizungumza na baadhi ya wazazi nao wamesema wanasikititishwa na hali hiyo  na kwamba wanajaribu kuwamiza wengine kutowaruhusu watoto kufanya biashara zisizowahusu katika kuwajengea maisha mema hapo baadaye.