WAZAZI NA WALEZI KUWASIMAMIA VIZURI WATOTO WAO KWA KUWEKA UZALENDO KWA NCHI YAO

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali zanzibar mh riziki pembe juma amewataka wazazi na walezi kuwasimamia vizuri watoto wao kwa kuweka uzalendo kwa nchi yao ili kuweza kupata maendeleo mazuri nchini.

Akizungumza na wazazi na walezi kwa nyakati tofauti wa wilaya ya mkoani na micheweni amesema maendeleo ya nchi hayaletwi na mtu kutoka taifa nyengine bali yanaletwa na mtu kutoka taifa husika, hivyo ni vyema kuwahimiza watoto wao kurudi nyumbani wanapomaliza masomo nchi ya nje ili kulitumikia taifa lao.

Mhe riziki amesema kuna tabia ya baadhi ya vijana wanapata nafasi za masomo nje ya nchi na baadae hawarudi kulitumikia taifa.

Aidha amesema serikali ya mapinduzi zanzibar inajitahidi kujenga skuli za kisasa ili kuwafanya watoto kusoma katika mazingira mazuri hivyo ni lazima kuwahimiza watoto wao kusoma.

Katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar dkt  idrisa muslim hija akizungumza katika mkutano huo amewataka wazazi kuwa na subra huku wizara hiyo ikiyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili.

Wakitoa maoni yao baadhi ya wazazi wamesema kuna tatizo la upungufu wa walimu hasa wa sayansi, hivyo wameishauri wizara ya elimu kulitafutia ufumbuzi tatizo la upungufu wa walimu pamoja na mrindikano wa wanafunzi madarasani.

Wakati huo huo waziri wa elimu na mafunzo ya amali mhe riziki pembe juma amefanya mkutano na walimu wakuu na kuwataka walimu hao kutimiza majukumu yao na kuwahimiza walimu wao kufuata maadili ya kazi ili kuleta maendeleo katika elimu.

 

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App