WAZAZI NA WALIMU KUSHIRIKIANA KATIKA KUIMARISHA KIWANGO CHA UFAULU WA WANAFUNZI

 

Naibu waziri wanchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali  za mitaa na idara maalum smz mh. Shamata shaame khamis amewataka wazazi walezi na walimu kuzidi kushirikiana katika kuimarisha kiwango  cha ufaulu  wa wanafunzi.

Amesema kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kikiwa kikubwa taifa litakuwa na uhakika wa kuwa na wataalamu wengi ambao ni muhimu katika kuleta maendeleoya nchi.Mh shamata ameyasema hayo huko amani katika sherehe ya kuwakabidhi zawadi  wanafunzi ishirini na moja waliofanya vizuri kwenye  mitihani yao  katika skuli mbali mbali  za zanzibar.

Amesema katika kuhakikisha wanafunzi  wanafaulu vizuri lazima  kuwepo ushirikiano mzuri miongoni  mwao na kuondosha changamoto  zilizopo katika skuli na kuahidi kupigania kuongezwa kiwango cha mishahara  kwa walimu wa skuli za maandalizi.Mwalimu  mkuu wa skuli hiyo ndugu amesema skuli hiyo imekuwa ikishika nafasi ya tano mkoa  kwa kufanya vizuri mtihani ya taifa.Naye   bi asiya  khamisi mussa  kwa niaba ya mkurugenzi idara ya elimu  zazibar  amesema serikali imeandaa sera mathubuti  ya maandalizi na skuli za msingi  hivyo ni vyema walimu kujituma kwa bidii ili kuongeza kasi ya ufaulu mzuri.