WAZAZI NCHINI WAMESHAURIWA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA MITI SHAMBA

 

Wazazi  nchini wameshauriwa kuacha kutumia dawa za miti shamba na wafuate maekezo wanayopatiwa na wataalamu wa afya wakiwemo wauguzi  na wakunga ili kuepusha matatizo mbalimbali yanayoweza kujitokeza.Akizungumza na zbc ikiwa ni shamra shamra za siku ya maadhimisho ya wakunga dunia muguzi na  mkunga mkuu wa hospitali ya kivunge bi mwanamvua said amesema utumiaji wa dawa za miti shamba husababisha  kuharibika kwa fuko la uzazi na kutokwa damu nyingi hali ambayo inaweza kutopoteza maisha kwa mama na mtoto.

Aidha  mkunga huyo amewaomba wazazi kujifungulia katika vituo mbalimbali vya  afya ili kuweza kupatiwa matibau ya haraka  pale wanapopata matatizo.Kwa upande wao wazazi hao wamewashauria wazazi wenzao kuacha tabia ya kutupa taka ovyo  katika wodi kwani kunaweza kuleta  maradhi kwao wao na watoto.Mapema  msaidizi mkurungezi wa huduma za waauguzi na wakunga   hospitali ya mnazi  mmoja  asha msenga mrisho akizungumza na wazazi hao katika wodi hizo amewaomba wazazi hutoa ushirikiano katika kufanikisha siku ya wakunga duniani na kuwaomba kutoacha kuhudhuria vituo cha afya kabla na baada ya kujifungua .katika  kufanikisha shughuli hizo walishiriki pia wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali  kwa kutoa huduma na kuangalia afya za akina mama na watoto waliojifungua na wasio jifungua.