WAZAZI WAMELALAMIKIWA KUTUPA TAKA OVYO NYUMA YA MADIRISHA

 

Baadhi ya wazazi wanaokwenda kujifungua katika hospitali ya manzimmoja jengo la dodoma wamelalamikiwa kutupa taka ovyo nyuma ya madirisha na kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Meneja wa majengo  ya hospitali na mkuu wa usimamizi wa usafi abdi foum na mhudumu  wa usafi  salama abdi yussuf, wakizungumza na zbc kwenye zoezi la usafi lilowashirikisha asasi  ya vijana ya umoja wa mataifa (unc) ya chuo cha  utawala wa umma ipa, wamesema tabia hiyo haikubaliki na kuonya wasiendelee kufanya hiovyo.

Wamesema kila eneo la hospitali hiyo kumewekwa vifaa maalum vya utupaji wa taka lakini inashangaza  kuona baadhi ya wagonjwa kutovitumia  vifaa hivyo na badala yake  kutupa taka kupitia kwenye  madirisha.

Waaandalizi wa zoezi hilo la usafi  asasi ya vijana ya umoja wa mataifa (unc) ya chuo cha utawala wa umma, wamesema lengo kuu la kufanya usafi ni kuazimisha miaka 54 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar ambayo yamewakomboa wazanzibari wakiwemo vijana.

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa wodi ya wazazi katika jengo hilo wamewataka wazazi wenye tabia hiyo kufuata kanuni za usafi kwa kuhakikisha wanatupa taka sehemu husika.