WAZAZI WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA WALIMU KUHAKIKISHA WATOTO WANAPATIWA ELIMU BORA

 

Wazazi na walezi  wametakiwa kushirikiana  nawalimu kuhakikisha watoto wanapatiwa elimu bora nyenye kiwango ili kuleta mabadiliko katika seka ya elimu nchini.

Hayo yameelezwa na waziri asiyekuwa na wizara maalum mh sira  ubwa mamboya  wakati wa kuweka jiwe la msingi ya skuli ya maandalizi   huko ndijani  muembe punda  ambao  ujenzi huo gharimu  zaid  shilingi  milioni thalathini na tano na kuchangiwa na wananchi, halmashauri  muakilishi  na viongozi mbali mbali    ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra  ya madhimisho ya miaka hamsini ya mapinduzi ya zanzibar .

amesema elimu ni ufunguo wa maisha hivyo lazima wazazi kushirikiana na walimu kwa kuweza kuwafatilia nyendo zao  na tabia  nyema na kuahidi kuchangia shilingi milioni saba kwa kukamilisha ujenzi huo.

naibu waziri wa elimu mh  mmanga mjawiri   amesema walimu wanapaswa kuwafundisho maadili mema  wanafunzi .

Amesema  atahakikisha kuzitembelea skuli zote ili kuangalia maendelea ya wanafuzi katika kutatua changamoto mbai mbali .

Mkuu wa mkoa wa kusini mh hassan khatibu  amesema katika wilaya ya kati anaskuli hamsini na nne   na kutaka walimu na wazazi kuleta mabadiliko .