WAZIRI AAGIZA KUBUNIWA NJIA ZA UWEKEZAJI ZITAKAZOWEZA KUWAVUTIA WAGENI

 

 

Waziri wa habari, utalii na mambo ya kale mh mahmoud thabiti kombo ameiagiza jumuiya ya wenye mashamba   kijiji cha jozani (uwemajo)  kuangalia uwezekano    wa kubuni  njia nyengine zaidi za uwekezaji zitakazoweza kuwavutia wageni wanaotembelea  katika  maeneo yao.

Amesema pamoja na  jumuiya hiyo kujishuhulisha na  ufugaji wa viumbe vya bahari kwa kutumia mabwawa  na ukulima,  lakini bado   wanahitaji  njia nyengine za kuwekeza  ili waweze kujipatia kipato zaidi.

Waziri wa habari ametoa agizo hilo  katika sherehe   za uwekaji wa  jiwe la msingingi  za uanzishwaji wa kilimo cha kisasa kwa kutumia shamba la kitalu(green house)  zilizokwenda sambamba na uzinduzin wa jarida la  la jikomboe na umasikini zilizofanyika   jozani.

Mkuu wa mkoa wa kusini unguja  mh hassan khatib hassan amesema   kwa kuwa msitu una nafasi nzuri  na ni fursa pekee ya kukuza utalii hivyo     watahakikisha    wanayatumia vyema mazingira ya maeneo  ya hapo  ili waweze kuingia katika ushindani wa utalii kwa wote.

Katika risala ya wanajumuiya hiyo wamesema lengo lao kubwa ni kuisaidia wanajamii  hasa wakulima wa kijiji cha jozani  kuwa na sauti moja za kutafuta mbinu mbada la kiuchumi baada ya kushindwa kuyatumia  vyema mashamba yao ipasavyo kutokana na kuharibiwa na wanyama aina ya kimapunju ambao wanayazunguka maeneo hayo.

Katika hafla hiyo waziri  wa habari alizindua   kilimo  cha mboga mboga  kinachotumia   mbinu za kisasa  ambacho mazao yake hayawezi kuharibiwa   na wanyama pamoja na kuzindua  kijarida  kilichoandikwa jikomboe.