WAZIRI MKUU MAJAALIWA AMEWAONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA KOROGWE

 

Waziri mkuu kassim majaaliwa leo amewaongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa korogwe vijijini  mh. Khalidi hillary ngonyani  maarufu kwa jina la profesa maji marefu aliyefariki  julai  2 katika hospitali ya taifa ya muhimbili  ya jijini dear es salaam  alipokuwa amellazwa akipatiwa matibabu  .

Mwili huo uliagwa katika viwanja vya karimjee ambapo viongozi mbali mbali walihidhuria wa vyama  vya siasa na serikali pamoja na wabunge  wakiwemo spika wa bunge job ndugai ,naibu spika dk. Tulia akson ,katibu mkuu wa chama cha mapinduzi  dk. Bashiru ali .

Akitowa salamu za rambi rambi   kwa niaba ya serikali waziri mkuu kassimu majaliwa ameitaka familia ya  marehe mu ngonyani  kuishi  kwa pamoja na upendo bila ya kufarikiana pia amesema kuwa mh. Ngonjani ni mbunge ambae alikuwa mstari wa mbele kuwapigania wananchi  wa mkoa wa tanga.

Nae spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania  mh. Job ngugai na spika mstaafu wa bunge lililopita mh. Anne makinda  wote kwa pamoja walimuelezea marehemu ngonyani    alikuwa ni mtu aliyeipenda sana kazi yake   ya kuwatumikia watu wa korogwe  na kusema  wananchi hao wamempoteza mtu muhimu sana.

Akitowa salamu za rambi rambi katibu mkuu wa ccm dk. Bashiri ali amesema marehemu ngonyani amekufa wakati akitekeleza  ilani ya ccm  hivyo amewataka watanzania kuungana   kwa umoja  katika kuendeleza kutekeleza yale meema aliyoyaacha .

Arehemu halidi hilali  ngonyani maarufu kwa jina na profesa maji marefu amezaliwa tarehe 25mwezi  5 mwaka 1956 katika wilaya ya songea mkoani ruvuma ameacha wake na watoto mungu alilaze  roho yake mahali pema  ameen.