WAZIRI MKUU WA INDIA NARENDRA MODI LEO AMEONESHA MATUMAINI KATIKA ZIARA YAKE

 

Waziri mkuu wa india narendra modi leo ameonesha matumaini katika ziara yake ya saa tatu katika ukingo wa magharibi  na kusema amani kati ya israel na palestina inaweza kupatikana mapema iwezekanavyo.

Modi amewasili ramallah akitokea jordan ikiwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi wa india kuzuru eneo hilo ambapo amekutana na rais wa mamlaka ya ndani ya palestina mahmoud abbas.Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari waziri mkuu huyo amesema amemuhakikishia mahamoud abbas kuwa india inaheshimu masilahi ya watu wa palestina.

Amesema ushirikiano wa india kwa palestina umekuwa ni suala la muda mrefu katika sera za india na kuwa ushirikiano huo hautayumba.Kwa upande wake rais mahmoud abbbas ametoa mwito kwa india kutoa mchango wake katika juhudi za kutafuta amani ya mashariki ya kati.