WAZIRI MKUU WA ISRAEL AMEMSIFU RAIS DONALD TRUMP KWA KUUTAMBUA MJI WA JERUSALEM KUWA MJI MKUU WA NCHI YAKE

Waziri mkuu wa israel benjamin netanyahu, anayefanya ziara katika umoja wa ulaya amemsifu rais donald trump wa marekani kwa kuutambua mji wa jerusalem kuwa mji mkuu wa nchi yake na kusema anatarajia mataifa ya ulaya kufanya kama hivyo.
Kabla ya mkutano wake na mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa ulaya mjini brussels, netanyahu amesema hatua ya trump, ambayo imeshutumiwa na wapalestina na serikali za mataifa ya umoja wa ulaya, itachangia katika kuleta amani katika mashariki ya kati.
Amewataka wapalestina kuitambua israel kama taifa la kiyahudi na kukubali kwamba jerusalem ni mji wake mkuu.
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa ulaya amesema kwamba mataifa ya umoja huo yataendelea kutambua msimamo wa kimataifa kuhusu jerusalem.