WAZIRI MKUU WA SERBIA VUCIC ASHINDA UCHAGUZI WA RAIS

 

Waziri Mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic ameibuka mshindi katika uchaguzi wa rais.

Vucic ameahidi kuendeleza jitihada za kujiunga na umoja wa Ulaya, lakini pia kuendeleza mahusiano na urusi pamoja na china.

Rais aliyepo madarakani Tomislav Nikolic, ambaye ni muasisi wa chama cha sns kinachoongozwa sasa na vucic, ameshinikizwa na waziri mkuu huyo na kuamua kutogombea muhula mwingine wa miaka mitano.

Vucic amesema kwamba atabaki kama waziri mkuu kwa miezi miwili ijayo muhula wa urais nikolic utamalizika mei 31 mwaka huu.