WAZIRI WA HABARI AMEHIMIZA UWAJIBIKAJI NA USIMAMIZI KATIKA UTENDAJI WA KAZI .

 

Waziri wa habari utalii na mambo ya kale mhe mahmoud thabit kombo amehimiza uwajibikaji na usimamizi katika utendaji wa kazi ili kuleta ufanisi.Waziri mahmoud ameeleza hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa shirika la utangaziji anzibar (zbc)  amesema iwapo kila  mmoja kwa anafasi yake atatekeleza wajibu wake ipasavyo kila jambo litakwenda vizuri na hakutokuwa na malalamiko .

Katika hatua nyengine amewahimiza viongozi wa shirika kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kufanyatathmini na kujadili masuala mbali mbali ya kiutendaji  .Mkurugenzi wa shirika la utangazaji bi ayman duwe amesema shirika  mashirikiano katika utendaji wa kazi ni jambo la muhumu na shirika limejipanga kufanya vitu vizuri zaidi kwa ajili ya watazamaji wake .Naibu katibu mkuu anaeshughulikia habari saleh yussuf mnemo pamoja na mwenyekiti wa boti wa shirika bi nassra mohamed hilali wamewataka wafanyakazi wa zbc kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwani ndio siri ya mafanikio katika kazi.