WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI REX TILLERSON AMETOA WITO WA KUFANYIKA UCHUNGUZI WA KINA

Waziri wa mambo ya nje wa marekani rex tillerson  ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina kuhusiana na tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya waislamu wa jamii ya rohingya nchini myanmar.

Tillerson ameyasema hayo mara baada ya kukutana na kiongozi na raia wa myanmar pamoja na viongozi wa kijeshi nchini humo.

Zaidi ya waislamu wa jamii ya rohingya laki 6 wameikimbia nchi hiyo na kwenda nchi jirani ya bangledesh kufuatia operesheni inayojulikana kama safisha safisha inayoendeshwa na jeshi katika jimbo la rakhine nchini humo.

Tillerson ambaye amekuwa na mazungumzo na kamanda wa vikosi vya myanmar amesema kuwa marekani bado inachunguza iwapo operesheni hiyo inapaswa kutambulika kama operesheni safisha safisha na kuongeza kuwa kwa sasa haoni haja ya kuiwekea vikwazo vya kiuchumi myanmar ingawa hatua za aina hiyo zinaweza kuchukuliwa kwa mtu mmoja mmoja.