WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UFARANSA AMEIZURU IRAQ

 

Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, ameizuru iraq ili kuzungumza na maafisa wa nchi hiyo kuhusu hatua ya kuijenga upya iraq iliyotangaza ushindi dhidi ya kundi linalojiita dola la kiislamu is.

Akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa baghdad, waziri huyo  amesema lengo la ziara yake ni kuelezea uungaji mkono wa ufaransa kwa iraq.Waziri huyo wa mambo ya nje wa ufaransa ameongeza pia kuwa nchi yake itaendelea kuhudumu kwenye muungano wa kijeshi na kushiriki kwenye hatua ya ujenzi mpya wa taifa hilo lililoharibiwa vibaya kwa vita.

Ufaransa ilishiriki katika operesheni dhidi ya is iliyoongozwa na marekani baada ya kundi hilo kunyakua sehemu kubwa ya iraq na nchi jirani ya syria mwaka 2014.Iraq inatazamia kupata fedha katika mkutano wa ujenzi mpya wa nchi hiyo unaofanyika kuwait kuanzia leo hadi jumatano.