WHO KUCHUKUA TAHADHARI KUZIMA MLIPUKO WA UGONJWA HATARI WA EBOLA

 

Shirika la afya duniani, who limeahidi kuchukua hatua za tahadhari na haraka za ili kuzima mlipuko wa ugonjwa hatari wa ebola kaskazini mwa jamuhuri ya kidemokrasi ya congo.

Shirika hilo limesema limetuma wataalamu maeneo ya vijijini, kunako aminika kutokea visa 11 vya ugonjwa wa ebola — zikiwemo ripoti ya vifo vya watu watatu.

Who inafanya kila mbinu kubaini ukubwa wa mlipuko wa ugonjwa huo, kutoa tiba walioambukizwa na kuwatambua walioambukizwa au watu waliokaribiana na walioambukizwa virusi hivyo.

Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa ebola nchini congo, tangu kisa cha kwanza kutambuliwa la nchini humo mnamo mwaka wa 1976.