WHO KUWEKA MIKAKATI WA KUHAKIKISHA KUWA WANADHIBITI MARADHI YA MIRIPUKO

 

Naibu waziri wa afya mhe harous said suleiman amelitaka shirika la afya ulimwenguni who kuweka mikakati maalum wa kuhakikisha kuwa  wanadhibiti  maradhi  ya miripuko  hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa mrejesho wa maamuzi na maazimio ya mkutoano mkuu wa 7i wa  afya ulimwenguni uliofanyika geneva amesema mardhi ya kipindupindui, surua polio na malaria yanahitaji mipango sahihi ya kupambana nayo ili   kuhakikisha maradhi haya yanaondoka kabisa.

Amesema kipambele cha wizara na serikali ni kumarisha huduma katika maeneo ya makundi maalum yakiwemo ya akina  mama , watoto na walemavu na wenye mahitaji maalum .

`naibu waziri wa afya tanzania bara dk faustine ndugulile amelitajka shirika hilo kwa mwaka ujao kuangalia maeneo ambao ni changamoto katika sekta ya afya na kwa jamii kwa ujumla ili kuweza kuyatatua .

Mwakilishi wa shirika la afya ulimwenguni  anaefanya kazi zake tanzania bara dk adiele onyeze amesem  katika kipindi kijacho wamnategemea kufanya mambo mengi katika sekta ya afya ambapo  husani kupamban ana maradhi hayo yanawasumbua sana wananchi.