WIZARA IMEANDAA MPANGO MKUU WA TAIFA WA UVUVI ZANZIBAR

Katibu mkuu wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi juma ali amesema wizara imeandaa mpango mkuu wa taifa wa uvuvi zanzibar ili kuwawezesha wavuvi kuvua katika bahari kuu.
Akifungua mafunzo ya uwasilishaji wa rasimu ya mapango huo, amesema wananchi wanashindwa kufikia malengo kutokana na ukosefu wa wataalamu na miundo mbinubora katika sekta hiyo.
Nd. Juma amesema kuwepo kwa mpango huo kutasaidia sekta ya uvuvi kukuwa zaidi kwani ndio sekta inayotegemewa katika kukuza uchumi ukilinganisha na kilimo ambacho kwa sasa maeneo yake yamevamiwa na ujenzi.
Aidha amesema rasimu hiyo inakwenda sambamba na mpango wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar ya kuimarisha sekta ya uvuvi ili kuondokana na uvuvi wa kujikimu na kwenda wa biashara.
Akiwasilisha rasimu hiyo kwa watendaji wa wizara hiyo na wadau mbali mbali wanaoshughulikia masuala ya uvuvi pro.beatus kundi kutoka chuo kukuu cha dar-es-salaam amesema iwapo mpango huo utakapokamilika utaweza kuisaidia wizara kufanya vizuri katika uendeshaji wa shughuli zake na kuongeza pato la serikali.
Hata hivyo ameishauri idara ya uvuvi kuendelea kutoa taaluma kwa jamii kwani imeonekana wengi wao kuwa na uwelewa mdogo wa kuahamu sheria za uvuvi na kushindwa kuzifanyia kazi ipasavyo.