WIZARA YA AFYA IIMEPANGA KUWASOMESHA MADAKTARI BINGWA WA MIFUPA

Wizara ya afya iimepanga kuwasomesha madaktari bingwa wa mifupa ikiwa ni juhudi za kukabiliana na upungufu wa madaktari wa kitengo hicho.
Naibu waziri wa wizara hiyo mh harous said amesema katika hatua ya awali itasomesha madaktari bingwa wawili na baadae itasomesha wataalamu wa kada nyengine
Akijibu swali katika baraza la wawakilishi amesema pia wizara imewapatia mafunzo madaktari wanne wa kawaida kutokana na ongezeko la ajali linalosababisha kuongezeka mahitajika ya huduma za uchunguzi na matibabu.
Wakati huo huo serikali imesema imeandaa utaratibu wa kuruhusu wafugaji kwenda kuwachukua wanyama wao waliochukuliwa kwa kutofuata sheria .
Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz mh haji omar kheir amesema katika utaratibu huo mfugaji atalazimika kulipa gharama za utunzaji wa wanyama wao kwa kipindi chote alichokuwa katika hifadhi ya serikali.