WIZARA YA AFYA IMEKABIDHI VIFAA VYA HUDUMA YA UZAZI

Wizara ya afya imekabidhi vifaa vya huduma ya Uzazi kwa halmashauri ya wilaya ya kati, ikiwa ni Utekelezaji wa upelekaji madaraka kwa wananchi Ugatuzi.Vifaa hivyo ambavyo ni msaada wa serikali ya canada kupitia shirika la idadi ya watu duniani unfpa, ni kwa ajili kuimarisha huduma ya mama na mtoto kwa wanakijiji unguja ukuu.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kati, mkurugenzi idara ya kinga na elimu ya aftya dk. Fadhil moh’d abdalla, amesema mfumo wa ugatuzi umepata nguvu zaidi baada ya jamii kuonesha matumaini ya kupata ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kati diwani wa wadi ya bungi nd. Said mtaji askari, amesema kupitia ugatuzi madiwani watakuwa na uwezo kufikisha mahitaji ya wanachi kwa haraka ili kupatiwa ufumbuzi.
Mratibu wa mradi wa afya bora ya mama na mtoto, bi sharifa awadh ameelezea umuhimu wa kutumika vyema kwa vifaa hivyo.