WIZARA YA AFYA KUHAKIKISHA WANANUNUA VIFAA MUHIMU VYA HOSPITALI

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi, ameuwagiza uongozi wa wizara ya afya zanzibar, kuhakikisha wananunua vifaa muhimu vya hospitali vitavyorahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
balozi seif ametowa agizo hilo, alipokuwa akizungumza na watendaji wa hospitali ya wete, mara baada ya kutembelea wodi ya wagonjwa ya akinamama chumba cha upasuaji na sehemu ya kuhifadhia dawa na kuchomea taka hospitali hiyo.
Amesema inasikitisha kusikia hospitali kubwa ya wete, inakosa vifaaa muhimu kama ultrasound mashine na bp mashine, vifaa ambavyo ni muhimu katika kufanyia uchunguzi wagonjwa kila wakati.
aidha balozi seif amewasisitiza watendaji hao kuwa na lugha nzuri wakati wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa, kwa kufuata maadili ya kazi na taaluma zao zinavyoelekeza na sio kuwatolea maneno yasiofaa wagonjwa.
Wakati huo huo balozi seifa amekabidhi vifaa mbali mbali vya hospitali na ameusisitiza uongozi wa wizara ya afya kuhakikisha wanawalipa wafanyakazi pesa zao za muda wa ziada wanazodai kabla ya kuondoka kisiwani pemba.
naibu waziri wa afya mh. Harous said suleiman na dk. Dhamana wa hospitali hiyo othman maalim wamempongeza balozi seifa kwa kuwapa msaada huo na kusema wanatatizo la ukosefu wa madawa na vifaa tiba.
vifaa alivyokabidhi katika hospitali hiyo ni pamoja na mashuka 50, mirija 500, ditoll galoni 9, vigari 5 na blangeti 9 ambapo balozi seif yuko kisiwani pemba kwa ziara ya siku mbili ya kutembelea miradi mbali mbali.