WIZARA YA BIASHARA VIWANDA NA MASOKO INAKUSUDIA KUYAONGEZEA UBORA MAZAO

wizara ya biashara viwanda na masoko inakusudia kuyaongezea ubora mazao ya biashara yanayosafirishwa nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya soko hilo

akizungumza katika kikao cha kujadili tafiti ya kuongeza ubora wa mazao hayo mkurugenzi mipango sera na utafiti wa wizara hiyo nana mwanjisi amesema kwa kushirikiana na wizara ya kilimo wataangalia njia bora za kuweza kuziboresha bidhaa hizo kuanzia hatua ya kilimo.

amesema utafiti huo ulioanza mapema mwaka huu kwa mazao ya viungo, karafuu na mwani unalengo la kuyaongezea ubora mazao hayo ili  kuhakikisha yanakuwa na nafasi katika soko la ulaya.

mkuu wa kitengo cha utafiti wa kilimo na biashara kutoka taasisi ya tafiti na mipango ya kudhibiti umasikini (repoa) gbadebo odularu amesema zanzibar inahitaji kuongeza thamani ya bidhaa zake hasa katika sekta ya kilimo ili kuweza kufikia mahitaji ya watumiaji wa soko la nje.