WIZARA YA ELIMU ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA MICHEZO

 

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh riziki pembe juma  amesema  wizara yake itaendelea kushirikiana na wizara ya michezo ili kuendeleza utamaduni  wa mzanzibari pamoja na kuinua vipaji vya watoto kwa kuandaa programu maalum ya sanaa na utamaduni.

amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha misingi itakayosaidia   udumishaji bora wa sanaa na utamaduni kwa watoto ili kuwasaidia kuitumia sanaa hiyo kuweza kujiajiri na kuajiriwa  na kuachana kutegemea ajira kutoka serikalini.

akizungumza na wanafunzi na walimu kutoka skuli mbali mbali katika muendelezo wa tamasha la 23 la mzanzibari linaloendelea mnara  wa kumbukumbu ya mapinduzi ya zanzibar  jamuhuri squar  mh pembe  ametoa  wito kwa  waandaaji wa tamasha hilo kuangalia uwezekano wa kuwa na programu za pamoja na walimu wa sanaa   zitakazosaidia kuwapa ujuzi walimu  ili kuibua vipaji zaidi.

Akimkaribisha mgeni rasmi naibu katibu mkuu  wa wizara ya vijana  utamaduni sanaa na michezo amour hamil bakar amesema  kazi kubwa iliyofanywa na wizara ya elimu kwa kushirikiana na wizara ya vijana   ndio  chachu ya mafanikio hayo  ya vipaji walivyoonyesha watoto  hao.

Kamishna wa utamaduni  wa wizara hiyo  shamuhuna amesema  idara ya utamaduni  itaendelea kukuza  na kuendeleza sanaa na utramaduni hasa kwa watoto ili kuwajengea mazingira mazuri ya kufahamu na kukuza vipaji vyao.