WIZARA YA KAZI IMEKUSANYA SHILINGI MILIONI MIA NNE NA MOJA, LAKI SABA SITINI SABA ELFU MIA SABA NA HAMSINI

 

Wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto imekusanya jumla ya shilingi milioni mia nne na moja, laki saba sitini saba elfu mia saba na hamsini hadi kufikia mwezi disembaAkijibu swali la mwakilishi wa jimbo la konde mh omar seif abeid, naibu waziri wa wizara hiyo mh shadya mohammed amesema fedha hizo  zimetokana na vibali vya kazi kwa wageni, mikataba ya ajira za nje, ada za usajili na ukaguzi wa vyama vya ushirika.

Aidha mhe, shadiya amesema fedha nyengine kati ya hizo zimekusanywa kutokana na ada ya ukodishaji wa ukumbi.Wakati huo huo naibu waziri wa wizara ya afya mh harusi said suleiman amewashukuru madaktari bingwa kutoka india walokuja zanzibar kusaidia kutoa matibabu..