WIZARA YA NCHI KUWAHAMISHA WATUMISHI 9710 KUANZA KUFANYA KAZI KATIKA OFISI ZA SERIKALI ZA MITAA

 

Wizara ya nchi, ofisi ya rais, tawala za mikoa, serikali za mitaa na idara maalum za smz, inatarajia     kuwahamisha watumishi 9710  kuanza kufanya kazi katika ofisi za serikali za mitaa kwa ajili ya ugatuzi ifikapo  mwanzoni mwa mwezi wa saba mwaka huu.Imesema  serikali  tayari imeshaanza kutekeleza  mpango huo  kwa kuanza kutumika ambapo fedha  za watumishi hao  tayari zimeshaidhinishwa   katika baraza hilo. akifafanua mpango huo  waziri wa wizara hiyo mh haji omar kheir amesema licha ya kuwepo baadhi ya  sera ambazo  zinahitaji kufanyiwa marekebisho  ili ziendane sambamba na masuala ya  ugatuzi.amesema   wizara ya  utumishi tayari imeshafanya mchakato  huo  wa kuwaorodhesha  watumishi  ambao watakuwemo katika zoezi la kugatuliwa.

Amefahamisha kuwa hivi sasa  ofisi ya rais tawala za mikoa    imo katika mchakato wa kuzipitia baadhi ya taasisi   vikiwemo vituo vya  kilimo, afya na skuli  ili kujua  idadi sahihi ya watumishi   ili kuepuka watumishi hewa kuingia katika mpango huo. akijibu hoja za wajumbe    naibu waziri wa wizara hiyo mh shamata shaame khamis amesema  licha ya mpango huo wa serikali  kukumbwa na changamoto lakini hautorejesha nyuma   katika utekelezaji wake. Mh shamata alikuwa akijibu swali la mwakilishi  wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini hidaya ali makame aliyetaka ufafanuzi  wa mpango huo katika ucheleweshaji wake.