WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS INA KUSUDIA KUANZA KUITUMIA SERA YA DIASPORA

Wizara ya nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ina kusudia kuanza kuitumia sera ya diaspora katika mwaka huu wa fedha.
Waziri wa wizara hiyo mh issa haji gavu amesema pia wanatarajia kutayarisha mpango kazi wa miaka mitatu ili kufanikisha utekelezaji wake ambapo pia inakusudia kuanza kuwaelimisha wananchi kuhusu sera hiyo.
Akiwasilisha bajeti ya wizara ya nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mh gavu amesema bajeti hiyo imeweka vipaumbele kadhaa ikiwemo kuendeleza ujenzi wa nyumba za ikulu, kuwahudumia wananchi kwa kutekeleza ahadi za rais pamoja na kutoa taarifa za shughuli za serikali.
Akiwasilisha maoni ya kamati ya kusimamia afisi za viongozi wakuu wa kitaifa makamo mwenyekiti wa mh panya ali abdalla amesahuri kufanyika utafiti utakaosaidia kuongeza mwamko wa wananchi wa kutumia fursa za mtengamano wa afrika wa mashariki.
Wajumbe mbalimbali wamechangia bajeti hiyo ya wizara ya nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ya mwaka 2017/ 2018.