WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO INATARAJIA KUFANYIA MATENGENEZO NYUMBA ZA MAENDELEO PEMBA

 

Wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji imeanza kuzifanyia matengenezo nyumba za maendeleo zilioko madungu chakechake

Akitoa taarifa ya ujenzi wanyumba hizo  kwa naibu waziri wa wiazara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji kaimu mkurugenzi  idara ya uratibu wa shirika la Nyumba Pemba  Suleiman  Hamad Omar  amesema  kufuatia uchakavu  uliopelekea kuanza kubomoka   nyumba hizo idara yake    itatumia shilingi milioni 62 kwa awamu ya kwanza ambazo zitatumika kulitengeneza block  moja lenye nyumba nane.

Kwa upande wao  wananchi wanaoishi katika nyuma  hizo wameishukuru serikali kwa juhudi zake  za kuwajali wananchi  kwa  kuwafanyia matengenezo nyumba zao kwani zilikuwa katika hali isiyoridhisha .

Nae  Naibu Waziri wa Wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji Mh: Mohd Ahmada salim amewataka wakaazi wa nyumba hizo kuzitunza kwa kuzifanyia usafi ili kuepuka maradhi ya miripuko ambapo kufanya hivyo ni kumuenzi muasisi wa ujenzi wa nyumba hizo marehemu mzee Abeid Amani Karume.