ZAECA IMEANDAA MPANGO MAALUM WA KITAIFA KUPAMBANA NA VITENDO VYA RUSHWA

 

Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi zanzibar  zaeca imesema imeandaa mpango maalum wa kitaifa wa kupambana na  vitendo vya rushwa  nchini utakaozinduliwa hivi karibuni.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo ndugu mussa haji ali ameelezea mpango huo katika mkutano wa mapambano dhidi ya rushwa na maadili ya viongozi zanzibar na kusema kuwa  mpango huo utakuwa shirikishi ambao utazihusisha taasisi za umma na  binafsi,  jumuiya za kiraia na watu wote katika jamii.

Profesa vicent kihiyo kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu ya sebastian kolwa amesema  malalamiko ya  rushwa yamekuwa mengi kutokana na watumishi wa umma  kukosa maadili   jambo linaloleta athari kubwa ndani ya sekta za kazi.

Akifungua mkutano huo katibu mkuu wizara ya kilimo,  maliasili mifugo na uvuvi ndugu joseph abdalla meza amesema jitihada nyingi zinatumika katika kusimamia maadili ya viongozi na kupiga vita vitendo vya rushwa ili kuwanusuru wafanyakazi na janga hilo.    

Tatizo la rushwa limekuwa kikwazo kwa zanzibar ikilinganishwa na tanzania bara kutokana na mamlaka hiyo kukosa uwezo wa kisheria wa kumfikisha mtuhumiwa katika   vyombo vya sheria.