ZAECA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA JAMII ILI KUVIFICHUA VITENDO VYA RUSHWA

Wananachi wa shehia ya kiwani wilaya ya mkoani wameitaka mamlaka ya kuzuia  rushwa na uhujumu wa uchumi zanzibar(zaeca) kuendelea kutoa elimu  kwa jamii ili kuwawaezesha  kushirikiana  katika kuvifichua  vitendo vya rushwa na uhujumu wa uchumi.

Wakizungumza na zbc baada ya kushiriki katika zoezi la utafiti sambamba na elimu  juu ya  madhara ya rushwa iliyotolewa na mamlaka hiyo, wananchi hao wamesema wakikabiliana na  vitendo hivyo katika maeneo tofauti ya utoaji wa huduma lakini kutokakana na ukosefu wa taaluma kuhusu athari na madhara ya rushwa hulazimika  kutoa rushwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma .

Akitoa tathmini ya utafiti huo  mdhamini wa zaeca pemba Suleiman Ame  Juma  amesema pamoja na mbinu waliyotumia  ya kutoa  elimu kwa mtu mmoja mmoja, lakini amewataka wananchi kuvitumia vyombo vya habari  ili kupata taarifa juu ya vitendo na athari zake.

Mamalaka ya kuzuia rushwa  na uhujumu  wa uchumi zanzibar imetoa elimu kwa wananchi  kupitia njia ya dodoso katika shehia ya makangale na kiwani kisiwani pemba.