ZAFELA KUITUMIKIA JAMII DHIDI YA VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UNYANYASAJI

Wasaidizi wa sheria wametakiwa kuyatumia vizuri mafunzo ya uandishi wa ripoti waliyopatiwa na kituo cha huduma za sheria wanawake (zafela) katika kuitumikia jamii dhidi ya vitendo vya udhalilishaji unyanyasaji ili kupatikane kwa taarifa zenye uhakika na kufanyiwa kazi kwa urahisi.
akifunga mafunzo ya siku mbili ya wasaidizi wa sheria wa wilaya tatu ambayo yameenda sambamba na kuwapatia compyuta 3 kwa wasaidizi hao yaliyofanyika ukumbi wa malaria mjumbe wa bodi ya wakurugenzi zafela bi hamisa mmanga amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuiwezsha jamii kutekeleza sheria.
Mratibu wa jumuia hiyo sada salum amewataka wakufunzi hao kuona umuhimu mafunzo hayo na kuviitumia vifaa hivyo kwa lengo liliokusudiwa ili kuleta ufanisi wa utendaji kazi.
Aidha washiriki wa mafunzo hayo wamesema yamekuja katika wakati muafaka kwani kwa mwezi uliopita wamezipokea kesi tano za udhalilishaji katika vijiji mbali mbali.