ZAIDI YA NYUMBA 80 ZIMEEZUKA MAPAA

Zaidi ya nyumba 80 zimeezuka mapaa na nyengine kuvunjika kufuatia upepo mkali uliovuma katika shehia ya pangawe, kinuni na nyarugusu.
Taarifa zinaeleza kuwa upepo huo umetokea majira ya saa tano za asuhuhi umesababisha hasara kubwa kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi wameelezea madhara yaliyowapata na namna ya upepo huo ulivyoanza.
Viongozi mbalimbali wametembelea maeneo hayo na kuwafariji kutokana na mkasa uliowapata na kuwataka kuwa wavumilivu.
Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi pia amefika katika eneo hilo na kusema kuwa serikali inafanya tathmini ya kuweza kuwasaidia wananchi hao kwani hasara waliyoipata ni kubwa.
Ameongeza kuwa si vyema wananchi wakaanza kuilaumu serikali badaya yake kushirikiana nayo kuona ni namna gani matatizo hayo yanatatuliwa.
Kufuatia tukio hilo ofisi ya mkuu wa mkoa wa mjini magharibi imekabidhi msaada wa chakula na kueleza kuwa na kueleza kuwa hiyo ni hatua ya awali kwa wananchi waliokumbwa na mkasa huo.