ZAIDI YA SHILINGI MILIONI AROBAINI ZIMETUMIKA KUNUNUNULIA VIFAA VYA MASOMO KWA WANAFUZI

 

Zaidi ya shilingi  milioni arobaini zimetumika katika nununulia vifaa vya masomo kwa wanafuzi wa skuli ya  msingi jendele  pamoja na skuli ya secondary  chwaka wilaya ya kati ikiwa ni kuwasaidia wanafunzi wanaosoma katika skuli hizo.

akikabidhi  vifaa hivyo bwana syafiq mobin kiongozi wa my  corps  zanzibar  mwalimu msaidizi skuli ya jendele amesema ataendelea  kusaidia  wanachi kwa  ajili ya maendeleo ya taifaili kuona elimu inakuwa kwa kasi.

Kwa upande wa skuli ya chwaka bwana  nurul asyikini kutoka my corps  pia amekabidhi mwalimu mkuu vifaa mbali mbali vya masomo kwa skuli ya sekondar chwaka .

naye  naibu sheha wa chwaka  omary iddi   na mwenyekiti wa jumuiya ya  wakulima na wafugaji  iddi haji jendele   meushukuru uongozi wa jumuiya ya muzdalifa ikishirikiana na my corps kwa msaada huo walioutoa  na kuwataka wasichoke kuwasaidia na wameahidi  kuutunza