ZAIDI YA SHILINGI MILIONI THAMANINI NA TATU ZINATARAJIWA KUTOLEWA MIRABAHA

 

zaidi ya shilingi milioni thamanini na tatu zinatarajiwa kutolewa mirabaha hivi karibuni na  afisi ya msajili wa haki miliki zanzibar
cosoza kwa wabunifu , wasanii na vikundi mbali mbali ,unguja na pemba ikiwa ni makusanyo ya kazi zao zinazotumika katika vituo vya
utangazaji na sehemu mbali mbali.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugawaji wa mirabaha hiyonaibu waziri wa vijana utamaduni sanaa na michezo  lulu msham juma amesema  makusanyo ya fedha hizo  ni zaidi ya  malengo ya ofisi hiyo kwa mwaka 2017-2018 walitakiwa kukusanya shilingi millioni 80.
Ameeleza kuwa kuwa  mgao huo ni wa awamu ya tano utakao wahusisha wasanii na wabunifu 1257 wa unguja na pemba utahusisha kasida,muziki,filam pamoja na maigizo.

nae naibu katibu mkuu wizara ya vijana utamaduni sanaa na michezo, amour hamil bakar ameeleza kuwa zoezi la ukusanyaji wa kazi za wasanii zinazotumika (mirabaha ) linakabiliwa matatizo mengi ikiwemo watumiaji wa kazi hizo kutokuwa wakweli katika ujazaji wa fomu za marejesho hali inayopelekea kukosekana kwa taarifa sahihi  na kupelekea ugumu wa ugawaji wa mirabaha.

Nae afisa mtendaji mkuu wa afisi ya msajili wa haki miliki  mtumwa khatib ameir amesema kazi za haki miliki ni biashara hivyo wanatarajia kufanya marekebisho ya kanuni ili kuwaingiza wasanii wote wenye vikundi wanaoimba kazi za wasanii wengine kibiashara.
Hivyo wamewataka watumiaji wa kazi za wasanii hasa vyombo vya habari kuzilipia ili kuwasaidia wasanii na wabunifu kukuza tasnia yao na kuchangia ipasavyo uchumi wa nchi.