ZAIDI YA TANI MIA MOJA ZA MCHELE AINA YA RED ROSE UMEZUIWA KUINGIA NCHINI

 

 

Zaidi ya tani mia moja za mchele aina  ya red rose umezuiwa kuingia nchini kutokana na kutokuwa na kiwango bora kwa matumizi ya binaadamu.Kaimu  mkurugenzi wa idara  ya  udhibiti usalama wa chakula  dk  khamis ali  omar  amesema  imekamata mchele  huo  katika  ukaguzi  wao wa kawaida katika   bandari  ya  malindi ukitokea  nchini  pakistan ambao  ni  mali  ya gago store.

Amefahamisha kuwa   baada ya kuufanyia uchunguzi wa   kimaabara  wamebaini kuwa mchele  huo haukidhi viwango kwa ajili ya mlaji pamoja na kuwekwa maandishi yasio sahihi.Mkuu  wa kitengo  cha uchambuzi na  athari  zinazotokana na chakula  aisha  suleiman  amebainisha  baadhi  ya  madhara  yanayojitokeza  dhidi  ya  matumizi  ya  vyakula  vibovu ikiwemo   maradhi sugu yatokanayo na kemikali  .Mchele  huo  zaidi ya tani mia moja uliingia nchini   ukitokea pakistani ambao  ulikusidiwa kwa soko la mauritius  na sio zanzibar ambao haukua na kiwango bora kwa matumizi ya binaadamu.