ZAIDI YA VIJANA 40 WAMEKUBALI KUACHANA NA DAWA ZA KULEVYA

Zaidi ya vijana 40 wamekubali kuachana na utumiaji dawa za kulevya kufuatia ziara ya mkuu wa mkoa wa mjini magharibi katika maficho ya vijana hao huko kinazini.
Vijana hao wametembelewa na mh ayoub mahmoud majira ya usiku ambapo baada ya kuwashauri wengi walikubali kaucha dawa hizo kwa hiari na kuanza tiba katika vituo vya kurekebisha tabia sober houses.
Katika usiku huo huo zaidi ya vijana 26 wamefikishwa kituo cha free at last na kupokelewa na ambao baadhi walitoa ushuhuda wa athari walilozozipata huku wakishukuru kupatiwa nafasi hiyo waliyoihitaji muda mrefu kwa kuwa dawa za kulevya zimeshawathiri kiafya, kiakili na kutengwa na jamii.
Mkuu wa kituo hicho junedi abdlkadir ameusifu uongozi wa mkoa mjini magharibi katika juhudi za mapambano ya dawa za kulevya.
Hata hivyo ameshauri kuendelezwa harakati zaidi za kusiaida wanaotaka kuacha dawa hizo kwani bado wapo wengi na wamekosa msaada.
Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi mh ayoub akizungumza na vijana hao amesema mkakati wa mkoa huo ni kukahakikisha biashara na utumiaji wa dawa za kulevya unamliza na kuwashauri kuwa tayri kuwataja wanajihusisha na biashara hiyo.
Mpango huo wa kuwasaidia vijana kuachana na dawa za kulevya ni miongoni kwa utekelezaji wa kampeni ya mimi na wewe ya mkoa wa mjini magharibi iliyozinduliwa hivi karibuni.