ZAIDI YA WAFANYAKAZI 40 WA WAMEANZISHA MGOMO WA SIKU MBILI

Zaidi ya wafanyakazi 40 wa kiwanda cha maji drop wameanzisha mgomo wa siku mbili baada yakutoona mabadiliko ya mshahara yao yaliyotangazwa na serikali kuu ya kima cha chini shilingi laki tatu.
Wakizingumza na zbc nje ya kiwanda hicho wafanyakazi hao wamesema wameanzisha mgomo huo kutoka na na uongozi wa kiwanda hicho kutotekeleza agizo la ongezeko la mshahara wa kina cha laki tatu.

Wamesema mbali na kugoma pia uongozi wa kiwanda hicho umekuwa na mashirikiano madogo na wafanyakazi ya maslahi muhimu na kwamba kumekuwa na manyanyaso mengi kiwandani hapo.

Aidha wameiomba serikali kuliingilia kati suala hilo ambalo kwa sasa umekuwa kero kubwa kwa wanyakazi hao.
Hata hivyo wamiliki wa kiwanda hicho hawakuwa tayari kuzungumza chochote kuhusu suala hilo.