ZAIDI YA WAKAAZI MIA SABA WANATARAJIWA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI

Zaidi wa wakaazi mia saba wa vijiji vya kianga mtendeni na mwera mtendeni wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi kufuatia kukamilika kwa vifaa vya kusambazia maji katika visima vilivyochimbwa ndani ya shehia hiyo.
Vifaa hivyo vimetolewa na manispaa ya magharib a kupitia mfuko wa mbunge wa jimbo, katika shehia zilizochimbwa visima ambavyo vinahitaji kukamilishwa
Wakaazi wa maeneo hayo wamesema kukamilika kwa vifaa vya kusambazia maji kutawaondoshea usumbufu wanaoupata kwa muda mrefu
Mbunge wa jimbo la mwera mh. Makame kassam makame na mwakilishi wa jimbo hilo mh. Mihayo juma nunga wamewasisitiza wananchi hao kuendelea kuwa wastahamilivu kupata maendeleo kwani uongozi unatambua matatizo yaliyomo katika jamii.
Maeneo ambayo tayari yameshachimbwa visima hivyo na kupatiwa vifaa vya kukamilisha upatikanaji wa huduma ya maji ni pamoja na shehia ya kianga mtendeni, mwera mtendeni na mji mwema katika jimbo la mwera na shehia za munduli na basra katika jimbo la mtopepo.