ZAIDI YA WATOTO LAKI MBILI WANATARAJIWA KUPEWA CHANJO ZA MATONE

 

zaidi ya watoto laki mbili wanatarajiwa kupewa chanjo za  matone ya vitameni ‘a’ na dawa za minyoo katika zoezi linalotarajiwa kuanza tarehe mosi juni  unguja na pemba.msimamizi wa lishe wilaya ya magharibi a’na b’ bi salama makame amesema zoezi hilo litawahusisha watoto wanaoanzia miezi sita hadi miaka mitano ambapo chanjo hizo zitatolewa katika vituo vyote vya afya .bi salama amewata wazazi na walezi  kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kupata chanjo hiyo ambayo  hazina matatizo yoyote kwa watoto na humuezesha  kukua vizuri kiafya na kiakili.amesema tokea kuaza kwa zoezi hilo mwaka 2007 vifo vya watoto vitokanavyo na  kukosa kwa vitameni ‘a’ na minyoo vimepungua kwa asilimi 33.amesema mafanikio makubwa yameweza kupatika kutokea kuanza kwa chanjo hizo ambapo hivi sasa imefikia asimia 98 ya watoto wanaopatiwa chanjo.