ZAIDI YA WATU 40 WAMEKUFA KATIKA AJALI YA TRENI MISRI

Zaidi ya watu 40 wamekufa wengine wengi wamejeruhiwa wakati treni mbili zilipogongana katika mji wa alexandria nchini misri. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kutokana na hali mbaya za majeruhi.
chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana lakini mwendesha mashitaka mkuu wa nchi hiyo ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusiana na ajali hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni misri imeshuhudia matukio kadhaa ya ajali za treni na ajali mbaya zaidi imetokea mwaka 2002 wakati treni moja ilipowaka moto na kuua zaidi ya watu mia tatu.