ZAIDI YA WATU 500 WAFA KWA EBOLA DRC

Wizara ya afya nchini jamhuri ya kidemokrasi ya kongo imesema imefika zaidi ya watu 500 waliofariki kutokana na virusi vya ebola. Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana imeeleza kuwa tokea kuibuka kwa ugonjwa huo mashariki mwa kongo, watu 505 wamekufa, na watu 271 wametibiwa. Ugonjwa huo ulizuka mwezi juni mwaka jana muda mfupi baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza kumalizika kwake katika eneo la magharibi mwa kongo. Kwa mujibu wa waziri wa afya wa nchi hiyo, oly kalenga, amesema tangu mwezi agosti, zaidi ya watu 70 elfu wamepatiwa chanjo ya ebola. Maafisa wa afya na mashirika ya kutoa misaada wamekuwa wakikabiliwa na matatizo katika kupambana na ugonjwa huo ikiwemo makundi mbali mbali ya wapiganaji yanaendesha operesheni zake, yakiwa yanagombania rasilimali za taifa hilo.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App