ZANZIBAR IMESITISHA KUTOA VIBALI VYA UINGIZAJI WA BIDHAA ZA NYAMA AINA YA POLYN NA SAUSAGE

 

 

 

 

 

 

wakala wa chakula na dawa zanzibar imesitisha kutoa vibali vya uingizaji wa bidhaa za nyama aina ya polyn na sausage zinazotoka kwenyekampuni enterprise food production na rainbow chichek limited za afrika kusini baada ya kuzuka ugonjwa wa listeria nchini humo.

kaimu mkurugenzi idara ya udhibiti usalama wa chakula kutoka wakala wa chakula na dawa dk. khamis ali omar amesema marufuku hiyo itadumu hadi hali ya usalama wa bidhaa hizo utakapothibitishwa na wizara ya afya ya afrika kusini.

amesema afrika ya kusini imeripoti kuzuka ugonjwa huo mwezi januari ambapo shirika la afya duniani who  limesema mripuko huo wa listeria ni mkubwa zaidi kwatika kumbukumbu za shirika hilo.

ugonjwa wa listeria unasababishwa na vimelea vya bakteria ambao hupatikana katika udongo, maji na mbogamboga  ambapo bidhaa za chakula zinazotokana na wanyama ziko katika hatari ya kupata vimelea hivyo.

khamis ametaja baadhi ya dalili za listeria ambao umeuwa watu 180 nchini afrika kusini ni kutapika, kkuharisha ukosa nguvu na maumivu ya mwili pamoja na maambukizi kwenye damu.

hivyo ametoa wito kwa wananchi kuchukuwa tahadhari kwa kuepuka kula vyakula vilivyokuwa havijachemshwa ili kujikinga na ugonjwa huo.