ZANZIBAR INA UWEZO MKUBWA WA KUPANDA MAPATO LAKE IKIWA LITAKUSANYA KWA UADILIFU

 

Waziri wa Fedha na mipango Dk. Khalid salum mohamed amesema zanzibar ina uwezo mkubwa wa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato iwapo wasimamizi wa sekta hiyo watafanya kazi kwa uadilifu.

Amesema kwa mujibu wa vianzio vya mapato vilivyopo upo uwezekano wa kukusanya shilingi bilioni 800 kwa mwaka na kutumika kwa masuala ya maendeleo.

Akizungumza kwenye kikao cha  viongozi wa taasisi za serikali katika ukumbi wa maktaba chake chake, dk. Khalid amesema wako baadhi ya walipa kodi hujenga urafiki na wasimamizi wa kodi ili kupata mwanya wa kutolipa kodi kwa mujibu wa sheria za kodi.

Aidha amesema ni jambo la kushangaza kusikia ofisi ya serikali imeshindwa kukusanya mapato kwa kipindi cha mwaka mzima huku ikiwa imepangiwa kukusanya kiwango cha fedha anachopaswa kuwasilisha serikalini.

Nae muhasibu mkuu wa serikali mwanahija almasi amewataka wakuu hoa wa taasisi za serikali kufuata mabadiliko ya ukusanyaji wa mapato na kuwa mstari wa mbele kusimamia matumizi ya fedha zinzokusanywa.

Akitowa neno la shukrani afisa mdhamini wizara ya ardhi maji nishati na mazingira juma bakar alaw wameahidi kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi ili kufanikisha azma ya serikali katika shughuli za maendeleo.